Taasisi ya Haki za Kiraia ya Wamarekani wenye Asili ya Kiarabu inamwakilisha Eyhab Aljabaly, ambaye anasema tukio hilo lilitokea mwezi Machi.
Kwa mujibu wa Aljabaly, mazungumzo yalianza kawaida kupitia ujumbe wa Facebook Marketplace hadi aliposema kuhusu kupanga kukutana na fundi wake.
Anasema kuwa mfanyakazi alijibu kwa ujumbe wa vitisho, akisema angefika “akiwa na silaha pamoja na binamu zake.” Aljabaly alisema baada ya hapo alielezea dini yake, akieleza kwamba imani yake inakataza udanganyifu katika biashara. Anadai mfanyakazi huyo alimaliza mazungumzo ghafla akisema, “Ah, wewe ni Mwislamu? Mwisho wa mazungumzo.”
Baada ya kuripoti tukio hilo kwa uongozi, Aljabaly alisema mwanzoni walionekana kuwa na wasiwasi lakini baadaye walipuuza malalamiko yake. Anadai mfanyakazi huyo bado anaendelea kufanya kazi na kwamba uongozi wa kampuni hiyo ulikataa kushughulikia hali hiyo.
Alipoulizwa na FOX 2, mmiliki wa biashara hiyo ya magari, Jeff, alikana kabisa kuwepo matamshi ubaguzi, akieleza yeye pia ni mtu mwenye asili ya Kiarabu. Alisema kuwa ikiwa Aljabaly atatoa ushahidi wa ujumbe huo, mfanyakazi mtuhumiwa ataachishwa kazi.
Aljabaly alisema anatumai hatua za kisheria zitasaidia kuzuia matukio kama hayo kwa wengine. Kesi hiyo inatafuta uwajibikaji chini ya ulinzi wa haki za kiraia dhidi ya ubaguzi wa kidini.
342/
Your Comment